Friday, 24 June 2016

WAZIRI MKUU UINGEREZA AJIUZULU

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo mapema leo. Kiongozi huyo mkuu wa Nchi hiyo amechukua uamuzi huo baada ya Wananachi wa nchi hiyo kupiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya-EU na kushinda. Waziri mkuu Cameroon alikuwa akipiga kampeni ya kutaka nchi hiyo ibakie katika umoja huo, hivyo kitendo cha kutangaza kujiuzulu ni kufuatia kushindwa huko katika kura hiyo na sasa Uingereza itajitenga rasmi na umoja huo. Awali Cameroon aliwaonya raia hao kuhusiana na maamuzi yao kuwa yataghalimu vizazi na vizazi vya Taifa hilo kwani wakishajiondoa kurudi itakuwa ngumu. Mgombea Uraisi wa Marekani Donard Trump amefurahishwa na kitendo cha uingereza kujitoa na kuitaka iharakishe haraka hatua za mwisho za kuondoka katika umoja huo. Hata hivyo, Trump hajaelezea sababu za kufurahishwa kwake wala sababu za kuitaka iharakishe kuondoka katika Umoja huo.

No comments:

Post a Comment