Wednesday, 1 June 2016

MBOWE"TUKO TAYARI KUTIMULIWA WOTE BUNGENI

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema wako tayri kutimuliwa wote Bungeni. Mbowe aliyasema hayo jana wakati akiwaongoza Wabunge wa upinzani kutoka ktk ukumbi wa bunge ikiwa ni mkakati wa kupinga Naibu Spika kuongoza Mjadala Bungeni hapo. Hali hiyo imeibuka juzi baada ya Naibu Spika kuzuia mjadala wa wanafunzi waliofukuzwa UDOM kujadiliwa.Mbowe amesema kuwa wako tayari kutimuliwa wote kwani siasa zinaweza kufanyika hata nje ya Bunge. Mh. Mbowe anayazungumza haya siku moja baada ya kufukuzwa wabunge 7 wa upinzani bungeni kutohudhuria vikao basdhi vya bunge kwa madai ya kufanya vurugu mwez Januari wakati waMjadala wa kurusha Matangazo ya Bunge moja kwa moja kupitia shirikala Utangazaji laTaifa TBC1. Waliosimamishwa vikao vya bunge Ni Tundu Lisu, Halima Mdee, Ester Bulaya, Zito Kabwe, Godbless Lema, John Heche pamoja na Paulina Gekul, ambapo kati ya Hao Chadema ni 6 huku mbunge Pekee wa Chama cha ACT- wazalendo Zitto Kabwe naye akitimuliwa na kutimiza Idadi ya wabunge saba.

No comments:

Post a Comment