Wednesday, 1 June 2016

MAGUFULI: TUTAKOMESHA NA KULIMALIZA KABISA TATIZO LA WATUMISHI NA WANAFUNZI HEWA.

Rais wa Tz Dk. John Magufuli amesema serikali ya awamu ya tano imepanga kurekebisha makosa yote yaliojitokeza huko nyuma likiwemo tatizo la watumishi hewa na wanafunzi hewa litaliloibuka hivi karibuni. Rais amewataka watanzania kutoingiza siasa ktk masuapa nyeti kama ya elimu kwani yakiachwa yaendelee Taifa litazalisha watu wa Ajabu. Rais ameaema kuwa anashangazwa na watanzania wa kidato cha nne kusoma shahada wakati yeye anachojua ni mtu kuanzia astashahada,stashahada na baadae shahada. Rais anayazungumza haya ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Elimu kuivunja bodi ya TCU kutokana na kudahili kimakosa wanafunzi wapatao 496 ktk chuo kikuu cha Mt Joseph kusomea shahada ya Sayansi ya Elimu huku wakiwa hawana sifa. Juzi katibu mtendaji wa TCU aliyesimamishwa kazi Prof. Mgaya alivipaumu vyombo vya habari vilivyokuwa vikihoji hatua ya Serikali kumsimamisha akisema Serikali inadhamira nzuri ya kuhakikisha Taifa linakuwa na elimu bora hivyo hatua ya waziti ilikuwa sahihi.

No comments:

Post a Comment