Wednesday, 13 July 2016

MAREKANI KUONGEZA ZAIDI WANAJESHI, SUDANI KUSINI

Marekani imesema itawatuma wanajeshi 40 zaidi Sudan Kusini kusaidia kulinda Wamarekani na mali ya Marekani mjini Juba. Msemaji wa jeshi la Marekani barani Afrika, Africom, Jennifer Dyrcz amesema wanajeshi hao wa Marekani wametumwa nchini humo baada ya mapigano yaliyoanza wiki iliyopita. Kwa sasa hali imetulia baada ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kuagiza wanajeshi wao wasitishe vita Jumatatu. Ubalozi wa Marekani mjini Juba, kwa mujibu wa shirika la habari la AP, umesema raia wa Marekani wanaotaka kuondoka Sudan Kusini watasaidiwa kuondoka kwa ndege. Wafanyakazi wasio muhimu sana katika ubalozi huo pia wataondolewa. Museveni atuma jeshi kuokoa waganda Sudan Kusini Utulivu warejea Juba, Sudan Kusini Mashirika makubwa ya ndege yalisitisha safari za ndege kutua na kupaa kutoka Juba. Safari za ndege za kibinafsi na za kukodisha hata hivyo zimerejelewa na ndege hizo zinatumiwa kuwaondoa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada pamoja na raia wa kigeni kutoka Juba. Umoja wa Mataifa umesema raia 36,000 wa Sudan Kusini wametoroka makwao kutokana na mapigano na kutafuta hifadhi makanisani, katika kambi za UN na kambi za mashirika ya kutoa misaada.

No comments:

Post a Comment