Thursday, 28 July 2016
CHUO KIKUU CHA SAUT CHAKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI DHIDI YA VYUO VYAKE VIKUU VISHIRIKI(MPEKUZI BLOG)
CHUO Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), kimetoa ufafanuzi wa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa vyuo vyake vishiriki vimezuiwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kufanya udahili wa wanafunzi.
Taarifa hizo zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimedai kuwa vyuo vishiriki vya SAUT ambavyo ni Stella Maris Mtwara University College (STEMMUCO) na Archbishop James University College (AJUCO) vimefungiwa na TCU kufanya udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT, Dk Thadeus Mkamwa, taarifa hizo ni za upotoshaji na kuwa hawajapokea taarifa kutoka TCU ikivizuia vyuo hivyo viwili kufanya udahili.
Aidha, Dk Mkamwa aliiomba jamii na wadau wa elimu kwa ujumla kupuuzia taarifa hizo kwa kuwa zina uwezekano wa kuwa ni mbinu chafu zinazofanywa na baadhi ya watu kuuhadaa umma hasa katika kipindi hiki ambacho ni muafaka kwa waombaji kufanya maombi katika vyuo vikuu.
“Tunauomba umma wa Watanzania kufahamu kuwa, Chuo Kikuu cha SAUT na vyuo vyake vikuu vishiriki vilivyotajwa hapo juu vinaendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/2017,” alisema Dk Mkamwa.
Alisema SAUT ni Chuo Kikuu kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania, na kwamba kimepiga hatua kubwa katika kujiendeleza na kufanikiwa kuanzishwa kwa vyuo vingine vikuu vishiriki vya SAUT ambavyo ni STEMMUCO kilichopo Mtwara, AJUCO kilichopo Songea na Jordan University College (JUCO) kilichopo Morogoro.
Vyuo vingine ni St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS)-Morogoro, Archbishop Mihayo University College (AMUCTA)-Tabora, na Cardinal Rugambwa Memorial University College (CARUMUCO) kilichopo Bukoba, Marian University College (MARUCO) kilichopo Bagamoyo.
Dk Mkamwa aliongeza kuwa, chuo kimeweza kuanzisha vituo vingine vitatu vya SAUT vilivyoko Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.
SAKATA LA KIJANA WA KITANZANIA KUTESWA NA MCHINA KATIKA MGODI HUKO GEITA HADI KUPOTEZA FAHAMU LACHUKUA SURA MPYA
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi, kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyodaiwa kufanywa na raia wa China wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro, Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni Watanzania.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa na hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa Tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo ya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.
Ilimlazimu Waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa Watanzania.
Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la Mtanzania kuteswa na mwajiri wake, kipigo kilichosababisha kupoteza fahamu na siyo kifo.
Hatua za awali Waziri Nchemba alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ya kushitakiwa na mwajiri wake kwa kosa la hatua zala kisheriaa wizi lililosababishwa apigwe.
Katika mahojiano ya Waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo, Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhusika hasa wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na akiwapo gerezani.
Katika hali hiyo, ilimlazimu, Mhe. Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwa ajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.
Katika oparesheni hiyo, kijana aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini Watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na Mchina mmoja walioshirikiana kumpiga, kumtesa na kumjeruhi.
Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika, Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na akaondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.
Katika hali nyingine ya kusikitisha, Waziri Nchemba amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa China katika mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa Geita zinaonesha raia 28 wenye vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo, lakini katika operasheni ya kushitukiza aliyoifanya Mhe. Nchemba amebaini uwepo wa raia wa china zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.
Hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa na kuchukuliw
Wednesday, 27 July 2016
BODI YA MIKOPO YATANGAZA MAJINA YA WANAODAIWA, ANGALIA KAMA NA WEWE UPO
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), inawaarifu wadaiwa wote ambao mpaka hivi sasa hawajaanza kulipa mikopo waliochukua kipindi wanasoma, na wenye majina yao kwenye orodha hii kwamba wamevunja mkataba kutokana na sheria ya bodi hiyo No. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) sehemu ya 19 (1).
Na wanataarifiwa kwamba, kulingana na sheria hiyo ya bodi (HESLB) No. 9 ya 2004, Bodi imedhamiria kutenda yafuatayo:-
(i) Bodi itachukua hatua za kisheria kulingana na kipengele cha 19 (a) (1) cha sheria ya bodi.
(ii) Mdaiwa atapewa penati ya 5% juu ya ile 5% iliyokua ikitozwa kabla kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo.
(iii) Mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni zilizoingiwa na bodi.
(iv) Mdaiwa atawekwa kwenye ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.
(v) Mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa Serikali au udahili wa masomo ya juu kwenye vyuo vyovyote ndani na nje ya nchi.
(vi) Maelezo yao yatapelekwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani, kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi.
Wadaiwa wote ambao majina yamechapishwa kwenye magazeti na kwenye tovuti ya bodi ya mikopo (Bonyeza hapa kuyasoma majina hayo) wanatakiwa kulipa madeni yao mapema iwezekanavyo kuzuia wao kupata adhabu hizo zilizotajwa hapo juu.
MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA YATOA HUKUMU YA MAUAJI YA SAIDI MWANGOSI
Leo July 27 2016 Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imetoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha Television cha chanel Ten, Daud Mwangosi.
Mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 mshtakiwa wa mauaji hayo, askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’ Pacificius Simon.
Hukumu hiyo imekuja baada ya juzi mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 2012 kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi wakatia CHADEMA ikifanya uzinduzi wa matawi, huku kukiwa na katazo la mikutano au makusanyiko ya kisiasa kutokana na seriakali kuongeza muda wa sensa ya watu na Makazi.
BASATA YAMFUNGIA NEY WA MITEGO KWA MUDA USIOJULIKANA.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.
Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.
Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.
Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na; 1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA. 2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.
3. Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake.
Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI Godfrey L. Mngereza KATIBU MTENDAJI, BASATA.
Friday, 22 July 2016
UAMUZI WA BODI YA MIKOPO KUHUSU WADAIWA AMBAO HAWAJAREJESHA MIKOPO YAO HADI LEO
Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na: Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu yajuu
SERIKALI KUFUTA DEGREE HEWA VYUO VIKUU.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kufuta programu zinazotolewa na vyuo vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
“Wakati mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.
Aliendelea kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.
Aidha Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.
Wakati huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha nia ya kujiunga katika Chuo hiko.
Vile vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.
Kwa upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato sita.
Maonyesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu wake.
Thursday, 21 July 2016
NCCR MAGEUZI WAANZA KUSHIKANA UCHAWI, MAKAM MWENYEKITI ATIMULIWA UANACHAMA...MBATIA ANENA YA MOYONI
Chama cha NCCR – Mageuzi kimemvua uanachama makamu mwenyekiti wake (Bara), Leticia Ghati (pichani) kikimtuhumu kujihusisha na migogoro ndani ya chama na tuhuma nyingine za kijinai.
Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa uamuzi huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Mbunge huyo wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema makosa mengine aliyokutwa nayo Ghati ni pamoja na kukashifu na kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama nje ya utaratibu na kuhujumu chama wakati wa uchaguzi.
“Kwa makosa hayo ambayo Leticia Ghati aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua uanachama,” alisema Mbatia.
Mustakabali wa chama Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake.
“NCCR tutahakikisha Ukawa unaboreka na kusimama imara kwa ajili ya kupata Katiba, tumeazimia kuunga mkono jitihada za kuunganisha vyama vinavyounda umoja huu ili kufikia lengo la kuwa na chama kimoja cha sias ala chenye nguvu,” alisema Mbatia.
Mbatia pia alizungumzia hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini na kusema chama chake kimebaini kuwa taifa linaongozwa kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya kufuata Katiba, sheria na kanuni.
Alisema demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa na akatolea mfano mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha kikatiba chenye mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika uendeshaji wake kwa wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya Watanzania.
Alisema NCCR inakemea matu- mizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali.
“NCCR Mageuzi tunalaani tabia ya polisi kuwakamata na kuwahoji mara kwa mara viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa uhuru na haki za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao,”
PICHA ZA UCHI ZA MWANAMKE ALIZOPIGA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI CHUO KIKUU ZAVUJA WIKI MOJA BAADA YA NDOA NA MWANAUME MWINGINE
Kuna picha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mwanamke akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yote hayo yalitokea siku chache tu baada ya mwanamke huyo kufunga ndoa na mwanaume mwingine jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba iliyopita wakiwa chuoni na zimekuja kusambaa ndani ya wiki baada ya kufunga ndoa. Anadai kuwa ni kisasi cha ex wake aliyedhamiria kuivunja ndoa yake.
Akiongea kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha Ubaoni cha EFM kilichoruka Ijumaa iliyopita, mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo zimedhamlilisha mno kiasi cha kuiharibu ndoa yake, kuwaumiza ndugu zake na kuwakosea heshima wakwe zake na kwamba anajuta kupita kiasi.
“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema mwanamke huyo.
“Ni kitu ambacho kinaniuma na kimeniharibia mlolongo mzima wa maisha yangu, mpaka sasa hivi sielewi, mume wangu hawezi kunielewa tena na yeye ndio nimemwekea kama nguzo, ndio kila kitu kwasababu hata familia yangu hainielewi ,” ameongeza.
“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo, inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi kubwa,” alisema mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.
“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na moja mbili, ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana, nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”
“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.
Kwa mujibu wa best man wa harusi hiyo, waliziona picha hizo siku nne baada ya harusi wakati wanafungua zawadi walizopewa na kuzikuta zikiwa kwenye bahasha na kusababisha vita kubwa kwenye familia yao.
Anadai kuwa rafiki yake hataki kusikia chochote kuhusiana na kumsamehe mke wake na jitihada za ndugu kuwasuluhisha zimegonga mwamba.
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas.
Wednesday, 20 July 2016
BAVICHA WAIKIMBIA CCM DODOMA,SASA WATOROKEA DAR.
Wakati kukiwa na ulinzi mkali mjini Dodoma kuelekea Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limehamishia mkutano wake wa kamati ya utendaji jijini Dar es Salaam.
Jana, sekretareti ya CCM ilianza maandalizi kusafisha njia kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu uliopangwa kufanyika Jumamosi.
Awali, Bavicha ilikuwa imehamasisha vijana wa chama hicho kuja kwa wingi mjini hapa kwa ajili ya “kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa”, lakini Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifuta mpango huo akisema: “Waache wafu wawazike wafu wao”.
Pamoja na Mbowe kuzuia, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema wiki iliyopita kuwa wameandaa mkutano wa Kamati ya Utendaji wa Baraza hilo leo mjini Dodoma na ungefunguliwa na Mbowe.
Huku ulinzi ukizidi kuimarishwa, jana kulikuwa na uamuzi tofauti.
Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma, Malambaya Manyanya jana alisema wameamua kuuhamishia mkutano huo Dar es Salaam baada ya kuona mzozo umekuwa mkali.
"Tumeona mzozo ni mkali sana. Tumeona imeshakuwa shida, tukaona ngoja tukafanyie Dar,” alisema Manyanya.
Alisema wajumbe waliokuwa waingie Dodoma jana, wameambiwa wote waelekee Dar es Salaam kwenye jengo la makao makuu
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka yeye anasema kutakuwa ulinzi mkali na hakuna atakayeweza kujaribu kuvuruga mkutano huo ambao utashuhudia Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Ole Sendeka alisema kwenye ukumbi mpya wa CCM ambako ndiko mkutano huo utakafanyika, kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa ndani na nje ya ukumbi ili kuwezesha kuona kila kitu kinachoendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, alisema ameona kwenye mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya vyama vinatoa vitisho na kuwataka wananchi wavipuuze.
“Na kama kuna mtu anadhani kuwa anaweza kukwamisha mkutano mkuu wa CCM, nimwambie Dodoma si salama kwake. Afikirie mahali pengine, lakini si Dodoma,” alisema.
“Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi pale wanapoona mtu wasiyemwelewa au dalili waripoti haraka kwenye vyombo vya habari na dola au kwa viongozi popote pale ambapo wanaweza kushirikiana kuliondoa hilo tatizo. Lakini kwa ujumla hali iko shwari mpaka sasa,” alisema Rugimbana.
Wakati Rugimbana akisema hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Mayalla Towo amesema wameweka miundombinu ya kuweza kuwabaini wahalifu, lakini hawezi kuitaja.
Tuesday, 19 July 2016
TCU KUFUNGUA MAOMBI YA VYUO VIKUU RASMI KESHO
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho.
Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31.
Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.
Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu.
Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
NDALICHAKO "HATUTATOA FEDHA ZA FIELD MPAKA ZOEZI LA UHAKIKI LIKAMILIKE"
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zitatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa wanafunzi waliombewa fedha hizo toka vyuo mbalimbali hapa nchini.
Prof. Ndalichako aliyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya ucheleweshwaji wa fedha hizo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
“Kuna zaidi ya wanafunzi 2,736 hewa ambao majina yao yamewasilishwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa ajili ya kulipwa fedha za mafunzo kwa vitendo, yakiwemo majina ya wanafunzi waliofariki na waliofukuzwa chuo,” alifafanua Prof. Ndalichako.
Aliendelea kwa kusema kuwa, kuna chuo ambacho kilituma ripoti ya wanafunzi waliofukuzwa chuo mwaka 2013/2014 lakini majina hayo yametumwa tena kwa ajili ya kupewa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa mwaka huu.
Kutokana na kasoro zilizojitokeza katika majina ya wanafunzi wanaotakiwa kupewa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo Prof. Ndalichako amesema kuwa Serikali haitatoa fedha mpaka uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo utakapo kamilika kwa vyuo vyote nchini.
Aidha, Mhe. Ndalichako amesema kuwa majina ya wanafunzi hao hewa yamewekwa katika mitandao wakitakiwa kujihakiki TCU ili kujiridhisha kama kweli ni wanafunzi na wanaendelea na masomo.
Vile vile, Prof. Ndalichako amevitaka vyuo vikuu kutoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa katika vyuo vyao kufanya uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo kwani kuna baadhi ya vyuo vimekuwa havitoi ushirikiano kwa kisingizio cha kuwepo kwenye mitihani.
Aliongeza kwa kusema kuwa, vyuo kutotoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa kufanya uhakiki wa wanafunzi hao kutazidi kuchelewesha fedha hizo kutoka mapema.
SERIKALI YATOLEA MAAMUZI SAKATA LA WALIOSIMAMISHWA UDOM MWEZI MAY, BAADHI KUREJEA UDOM
May 28 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma.
Wanafunzi waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 6,595 waliodahiliwa katika Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari na kundi la pili lilikuwa na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi.
Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako amesema kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanya Uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Baada ya uchambuzi huo leo July 19 2016 Serikali imetangaza maamuzi haya…….
Kundi la Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari Serikali imesema kwa kuwa uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II – 248), wanafunzi hao ndiyo pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili wakamalizie mafunzo yao katika Chuo hicho.
Wanafunzi 4,586 wa mwaka wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.
Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.
Wanafunzi 290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo nazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao.
Kundi la Programu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi Serikali imesema wanafunzi katika kundi hili hawakuwa sehemu ya program maalum ya kupunguza uhaba wa walimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati. Walikuwa wanaandaliwa kufundisha shule za msingi wakati lengo la Programu Maalum ilikuwa ni kukabiliana na tatizo za uhaba wa walimu wa Sekondari. Maudhui ya program waliyokuwa wanasoma hayakuwa sawasawa na yale ya Programu ya Ualimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi 29 wa mwaka wa II wenye Cheti cha Daraja IIIA waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi watahamishiwa katika Chuo cha Ualimu Kasulu wamalizie masomo yao kwa gharama zao wenyewe.
Wanafunzi 1,181 waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Kawaida ya Ualimu wa Elimu ya Msingi waombe mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo mahali popote watakapotaka wao.
Aidha Serikali imesema itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaorejeshwa UDOM na wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali watapewa mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya Ualimu itakayolipwa moja kwa mojachuoni.
Monday, 18 July 2016
UVVCCM: HATUWAONI BAVICHA DODOMA, VIJANA 3000 WATAHAKIKISHA USALAMA WA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU
Umoja wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.
Akiwa katika Ofisi za UVCCM –Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.
“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.
Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.
Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.
Sunday, 17 July 2016
TUME YA TAIFA YA VYUO VIKUU YATOLEA UFAFANUZI ALAMA ZA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MWAKA HUU 2016/2017
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa na vigezo.
Utaratibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Sifa hizo ziliwekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana. Taarifa hiyo inaonyesha kutolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Eliuta Mwageni.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku, alithibitisha taarifa ya utaratibu huo mpya.
Mkaku alisema utaratibu huo umetolewa baada ya mwaka jana kutumika mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ambao Januari, mwaka huu, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, aliagiza ufutwe na kurudishwa ule wa madaraja (division) uliotumika siku zote.
“Mfumo wa udahili uliotumika mwaka jana ulikuwa ni GPA na mwaka huu utatumika mfumo wa divisheni, ndiyo maana utaratibu huo ukawekwa,” alisema Mkaku.
Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo (2016/2017), ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa (D mbili) pointi 4.0.
Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokana na ufaulu wa A = 5; B= 4; C= 3; D = 2; E = 1.
Taarifa hiyo ilionyesha kuwa ili wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 wawe na sifa za kudahiliwa, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa (C mbili ) pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1.
Pia tovuti hiyo ilionyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu, watahitajika kuwa na ufaulu wa alama (D mbili) 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B = 4; C= 3; D= 2; E = 1.
Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne za D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A =75-100, B+ = 65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F= 0-38.
Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne za D za kidato cha nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) au Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Pia watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada (NTA) daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi (FTC) katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu, au wastani wa daraja la B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.
Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA.
Pamoja na hayo, TCU ilisema hakutakuwa na usajili wa mafunzo ya awali pamoja na yale ya UQF6 yaliyozuiwa kuanzia mwaka wa masomo wa 2016/2017.
Taarifa ya tovuti hiyo iliendelea kusema kuwa maombi yote ya usajili wa wanafunzi hao wanaotaka kuchukua shahada yanatakiwa kupitia TCU pekee.
“Kwamba tume hiyo imeamua kuwa kuanzia mwaka 2016/2017, maombi yote ya usajili kwa makundi yote yanayoanzia aya ya 3.0 kwenda juu wataunganishwa na TCU pekee na walio chini ya hapo hawatahusika na tume hiyo,” ilisema taarifa hiyo.
Pia TCU ilisema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kipengele cha 5(1)(c)(i) cha katiba ya vyuo vikuu, kifungu cha 346 cha sheria nchini.
“Msingi wa kubadili viwango vya kujiunga na elimu ya juu ni kutokana na kuwepo maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya uwezo wa wahitimu wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Mei, mwaka huu, Profesa Ndalichako aliwasimamisha kazi Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, kwa kushindwa kuisimamia tume hiyo kutokana na kuwapo kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa, kisha wakadahiliwa katika vyuo vikuu na kupata mkopo.
Wengine aliowasimamisha kazi ni Mkurugenzi wa Ithibati na Udhibiti Ubora, Dk. Savinus Maronga, Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka, Rose Kiishweko na Ofi sa Msimamizi Mkuu wa Taarifa, Kimboka Stambuli.
Saturday, 16 July 2016
BASATA YAUFUTA WIMBO WA NEY"PALE KATI PATAMU"
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.
ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo.
Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine.
Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
• BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rsmi kutumika kwa namna yoyote ile. • Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara kazi zao wanapotengeneza
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI, AGUSTINO MREMA WA T.L.P NAYE APEWA UONGOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Augustino Lyatonga Mrema.
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
2. William R. Mahalu
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
3. Mohamed Janabi
Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
4. Angelo Mtitu Mapunda
Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
5. Sengiro Mulebya
Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
6. Oliva Joseph Mhaiki
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
7. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
8. Charles Rukiko Majinge
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
9. Julius David Mwaiselage
Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Kupandishwa Vyeo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1. Essaka Ndege Mugasa 2. Adamson Afwilile Mponi 3. Charles Ndalahwa Julius Kenyela 4. Richard Malika Revocatus 5. Geofrey Yesaya Kamwela 6. Lucas John Mkondya 7. John Mondoka Gudaba 8. Matanga Renatus Mbushi 9. Frasser Rweyemamu Kashai 10. Ferdinand Elias Mtui 11. Germanus Yotham Muhume 12. Fulgence Clemence Ngonyani 13. Modestus Gasper Lyimo 14. Mboje John Shadrack Kanga 15. Gabriel G.A. Njau 16. Ahmed Zahor Msangi 17. Anthony Jonas Rutashubulugukwa 18. Dhahir Athuman Kidavashari 19. Ndalo Nicholus Shihango 20. Shaaban Mrai Hiki 21. Simon Thomas Chillery 22. Leonard Lwabuzara Paul 23. Ahmada Abdalla Khamis 24. Aziz Juma Mohamed 25. Juma Yussuf Ally
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1. Fortunatus Media Musilimu 2. Goyayi Mabula Goyayi 3. Gabriel Joseph Mukungu 4. Ally Omary Ally 5. Edward Selestine Bukombe 6. Sifael Anase Mkonyi 7. Naftari J. Mantamba 8. Onesmo Manase Lyanga 9. Paul Tresphory Kasabago 10. Dadid Mshahara Hiza 11. Robert Mayala 12. Lazaro Benedict Mambosasa 13. Camilius M. Wambura 14. Mihayo Kagoro Msikhela 15. Ramadhani Athumani Mungi 16. Henry Mwaibambe Sikoki 17. Renata Michael Mzinga 18. Suzan Salome Kaganda 19. Neema M. Mwanga 20. Mponjoli Lotson 21. Benedict Michael Wakulyamba 22. Wilbroad William Mtafungwa 23. Gemini Sebastian Mushi 24. Peter Charles Kakamba 25. Ramadhan Ng’anzi Hassan 26. Christopher Cyprian Fuime 27. Charles Philip Ulaya 28. Gilles Bilabaye Muroto 29. Mwamini Marco Lwantale 30. Allute Yusufu Makita 31. Kheriyangu Mgeni Khamis 32. Nassor Ali Mohammed 33. Salehe Mohamed Salehe 34. Mohamed Sheikhan Mohamed
Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.
Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam 16 Julai, 2016
MWANAFUNZI WA KWANZA KITAIFA ANATOKA SHULE YA KATA
Mwanafunzi aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Hassan Gwaay ameonesha moja kati ya tunda bora lililodhihirisha faida ya kuanzishwa kwa shule za kata na Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.
Gwaay mwenye umri wa miaka 19 ameeleza kuwa alisoma katika shule ya kata ya Mirerani Benjamin W. Mkapa mkoani Manyara alipopata elimu ya kidato cha nne na kupata ufaulu mzuri uliomuwezesha kuchaguliwa kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora (Tabora Boys) kuendelea na elimu yake ya kidato cha tano.
Amesema kuwa alipokuwa akisoma katika shule hiyo ya kata, wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule za watu binafsi zenye mazingira bora zaidi ya walikuwa wakimuonesha dharau lakini alitaka kuwadhihirishia kuwa hata katika shule hiyo anaweza kufanya vizuri zaidi yao.
“Sikujali kelele na dharau za watoto waliosoma kwenye shule za kulipia, ambao mara kwa mara walikuwa wakiibeza shule yetu. Nilopomaliza kidato cha nne, nilipata daraja la kwanza alama 10 (Division 1 ya point 10). Ndipo nilipowadhihirishia kuwa hata kwenye shule za kata watu wanafaulu,” Gwaay anakaririwa na gazeti la Jambo Leo.
Mwanafunzi huyo ambaye amelelewa na bibi yake kwa muda mrefu baada ya mama yake kufariki huku akiishi mbali na baba yake (anamsapoti), alisema kuwa baada ya kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora kusoma masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), aliweka bidii zaidi hasa baada ya kugundua kuwa wanafunzi aliokutana nao hapo wote walikuwa na akili sana.
Alisema kuwa alipofanya mtihani wa ‘Mock’ alipata Fizikia (A), Kemia (A) na Hesabu (B) na kwaba aliumia sana kuona amepata B. Aliongeza bidi hadi kuibuka na alama A kwenye mitihani yote katika Mtihani wa Taifa na kutangazwa kuwa mwanafunzi aliyeongoza.
Changamoto ya upungufu wa walimu hususan wa Sayansi ka.tika shule nyingi za umma nchini lilimkumba pia Gwaay katika shule ya wavulana ya Tabora, lakini aliipanda ngazi hiyo ndefu kwa nguvu ya ziada bila kukata tamaa.
“Hakuwa na Mwalimu wa Fizikia pale. Tangu najiunga sikuwahi kumwona zaidi ya wakuazimwa ambaye alikuwa akija jioni na mwisho mwa wiki tu na alikuwa akija mara chache. Muda mwingi tulitumia kujisome wenyewe lakini hatukukata tamaa,” alisema.
Shule ya wavulana ya Tabora mwaka huu imerudi kwenye nafasi yake ya ubora ulioaminika miaka mingi iliyopita. Imeshika nafasi ya 5 kati ya shule zote
Friday, 15 July 2016
UGAIDI: WATU 80 WAUAWA UFARANSA WAKISHEREHEKEA, RAIS WA NCHI HIYO AAPA KUTORUDI NYUMA
Watu 80 wameripotiwa kufa ikiwa ni pamoja na watoto 18 katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa jana katika mji wa Nice nchini Ufaransa.
Tukio hilo limetokea baada ya mtu mmoja mwenye bunduki aliyekuwa anaendesha Lori kuvamia katika eneo lenye mkusanyiko wa watu waliokuwa wakisherehekea maadhimisho ya Bastille ambapo mafataki mengi hurushwa.
Kwamujibu wa The Guardian, mshambuliaji huyo alirusha risasi kiholela (zigzag) akilenga kuua idadi kubwa zaidi kadiri awezevyo.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre, amesema Polisi walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua mshambuliaji huyo aliyeendesha Lori lake umbali wa kilometa 2 akitekeleza tukio hilo.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amelitaja tukio hilo kuwa baya la kigaidi na kuahidi kuwa nchi yake itakuwa imara na itapambana na magaidi ndani na nje ya mipaka yake. Alisema tayari ameamuru jeshi kuingilia kati kuwasaidia polisi hususan katika maeneo ya mipakani.
Hollande ameitisha mkutano wa dharura jijini Paris huku hali ya hatari dhidi ya mashambulizi ya kundi la Kigaidi ya ISIS ikiendelea. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kundi lolote lililobainisha kuhusika na tukio hilo.
SHULE 10 ZA KWANZA KITAIFA NA 10 ZILIZOSHIKA MKIA KITAIFA HIZI HAPA
Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) imetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016, na Kuzitaja shule zilizo fanya vizuri zaidi Kitaifa na zile ambazo hazikufanya vizuri Kitaifa.
Ubora wa shule umepagwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average –GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7.
Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:
==>Shule 10 Bora Kitaifa 1. Kisimiri (Government)
2. Feza Boys (Private)
3. Mwanza Alliance Girls (Private)
4. Feza Girls (Private)
5. Tabora Boys (Government)
6. Marian Boys (Private)
7. Kibaha (Government)
8. Mzumbe (Government)
9. Ilboru (Government)
10. Tandahimba (Private)
==>Shule 10 za Mwisho Kitaifa 1.Mpendae (Unguja)
2.Ben bella ( Unguja)
3.Tumekuja (Unguja)
4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)
5.Jang'ombe (Unguja )
6.Kiembesamaki (Unguja )
7.Tanzania Adventist ( Arusha )
8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )
9.Azania (Dar es salaam )
10: Lumumba (Unguja)
WATUMISHI WENGINE 3 POLISI MAKAO MAKUU WATUMBULIWA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya malipo hewa, yaani kulipa posho ya chakula (Ration Allowance) kwa watu ambao sio askari
Hatua hii ni mwendelezo wa uchunguzi wa tuhuma za kufanya malipo hewa ya kiasi cha sh. 305,820,000/= zilizopelekea kusimamishwa kazi kwa Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Bw.Frank Charles Msaki wiki iliyopita.
Kwa Mamlaka ya Katibu Mkuu chini ya Kanuni ya 35(2)(b) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Kuanzia tarehe 13 Julai, 2016, amewasimamisha kazi wafuatao: Bw. Damian Aloys Bupamba ambaye ni Mhasibu Daraja la II na Bi, Ida Dennis Moyo Mhasibu Daraja la I kwa makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Aidha kwa Mamlaka ya Katibu Mkuu chini ya Kifungu cha 7(4) cha Sheria Na.8 ya Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi na Magereza ya Mwaka 1990 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 8 ya mwaka 2015 kikisomwa pamoja na Kanuni C.23(1)(b) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995 zilizorekebishwa mwaka 2013, kuanzia tarehe 13 Julai, 2016, amemsimamisha kazi Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Milambo Mwita Milambo kwa makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Watumishi wote watatu wamehusika kufanya malipo haya jambo ambalo ni kinyume na Kanuni F.9 ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995 kama zilizovyorekebishwa mwaka 2013.
Katibu Mkuu amewasimamisha wahusika hawa ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma dhidi yao unaofanyika kufuatia Uchunguzi Maalamu wa Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi uliobaini makosa ya malipo hewa
BREAKING NEWS: Matokeo ya F6, Ualimu Msingi na Diploma Sekondari yametangazwa mda huu
Habari za hivi punde zinaarifu kuwa matokeo ya kidato cha Sita, Ualimu Msingi na Sekondari Diploma yametangazwa mda huu. Kwa maelezo zaidi tutakuletea ktk taarifa zetu hapahapa, usibanduke kwenda kusoma pengine, endelea kufatilia.
Thursday, 14 July 2016
PINGAMIZI LA LISU LAGONGA MWAMBA MAHAKANI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ya kufutiwa mashitaka ya uchochezi yanayomkabili na wenzake watatu.
Hakimu Mkazi Mkuu, Emillius Mchauru alitoa uamuzi huo jana baada ya kukubali pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri waliodai mashitaka hayo yasifutwe kwa kuwa hati ya mashitaka haina makosa.
Mbali ya Lissu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwandishi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob. Hata hivyo, uamuzi huo ulitolewa jana bila Lissu kufika mahakamani hapo kwa kuwa anaumwa.
Akiieleza mahakama, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai Lissu ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa, lakini wadhamini wake akiwemo Ibrahim Ahmed wamefika mahakamani na kueleza kuwa Lissu anaumwa malaria. Aidha, ilielezwa kuwa mshtakiwa Idrissa anaumwa na yupo Zanzibar kwa ajili ya matibabu.
Katika maombi yao, washitakiwa kupitia kwa Wakili Kibatala waliiomba mahakama ifute mashitaka hayo kwa kuwa hati ya mashitaka imekosewa kwa kutokueleza makosa hayo wametenda wapi na pia mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza masuala yanayohusu Zanzibar.
Akisoma uamuzi, Hakimu Simba alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote mbili katika kesi hiyo imejiridhisha kuwa hati ya mashitaka haina makosa.
Aidha, alisema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa makosa yaliyofanyika yanahusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivi karibuni, mahakama ilifuta mashitaka mawili ya uchochezi kati ya matano yanayowakabili washitakiwa hao, baada ya upande wa jamhuri kuyaondoa katika hati kwa kuwa hayana kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Katika mashitaka yao inadaiwa Januari 12 hadi 14, 2016, Dar es Salaam washitakiwa walichapisha taarifa ya uchochezi yenye kichwa cha habari ‘ Machafuko yaja Zanzibar’.
Pia inadaiwa Januari 14, 2016 Dar es Salaam walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar. Inaendelea kudaiwa siku hiyo hiyo, Lissu na wenzake bila ya kuwa na mamlaka yoyote yale waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar ili wasikubali kuingia kwenye marudio ya uchaguzi Mkuu.
RWANDA YATUPILIA MBALI MAOMBI YA ICC KUMKAMATA RAIS OMAR AL-BASHIR WA SUDANI
Serikali ya Rwanda imepuzilia mbali ombi la mahakama ya kimataifa ya jinai yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi ICC ya kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Rais Bashir atahudhuria kongamano la viongozi wa Afrika linaloandalia mjini Kigali wikiendi hii.
Rais Bashir atahudhuria kongamano la viongozi wa Afrika linaloandalia mjini Kigali wikiendi hii.
Waziri wa maswala ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa ombi la ICC kupitia kwa barua rasmi walioiandika siku mbili zilizopita haina uzito wowote.
Mapema juma hili mahakama ya ICC iliyashtaki mataifa ya Djibouti na Uganda kwa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kukosa kumkamata rasi Bashir alipozuru mataifa hayo.
Hii sio mara ya kwanza ziara ya rais Bashir imezua utata.
Mwaka uliopita mahakama ya Afrika Kusini ilimpata na hatia rais Jacob Zuma kwa kukiuka amri ya mahakama ya kumtia mbarano rais Omar el Bashir alipohudhuria mkutano wa umoja wa Afrika mjini Johannesburg nchini humo.
Waziri wa maswala ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo
Moja ya mada kuu katika kikao kijacho cha Kigali, itakuwa uhusiano baina ya bara la Afrika na mahakama hiyo ya ICC.
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakishikilia kukutu dhana kuwa dhamira kuu ya mahakama hiyo ni kuwahukumu viongozi wa Afrika ,huku viongozi wa mataifa ya magharibi wakiruhusiwa kuponyoka mkono wa sheria licha ya kuwepo kwa madai dhidi yao.
ICC iliyashtaki mataifa ya Djibouti na Uganda kwa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kukosa kumkamata rasi Bashir alipozuru mataifa hayo.
Mahakama hiyo kwa upande wake inasema kuwa imekuwa ikijaribu kutoa haki kwa maelfu ya waafrika ambao wamedhulumiwa.
ICC inamtaka bwana Bashir akamatwe kwa makosa ya mauji ya halaiki katika jimbo la Darfur Sudan.
Rais Bashiri amekanusha madai yote dhidi ya uhalifu huo.
BREAKING NEWS: ALSHABAB WAUA MAAFISA 4 WA POLISI NCHINI KENYA MDA MCHACHE ULIOPITA
Maafisa wanne wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mshukiwa wa ugaidi kumpokonya askari bunduki na kuwafyatulia maafisa wa Polisi.
Yamkini mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa amefungiwa korokoroni baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga na mtandao wa kigaidi wa Al Shabaab.
Alipelekwa katika kituo cha polisi cha Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
Awali gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi .
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea."
WANAFUNZI 2,739 WA ELIMU YA JUU WASITISHIWA MIKOPO
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha kwa muda mikopo kwa wanafunzi 2,739 walioshindwa kujitokeza wakati wa kuhakiki wanufaika wa mikopo hiyo.
Aidha, imetoa siku saba kuanzia jana kwa wanafunzi ambao hawakuhakikiwa kwenda kuhakiki katika vyuo vyao, vinginevyo mikopo yao itafutwa na kutakiwa kurejesha kiasi walichokopeshwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Jerry Sabi, alisema hatua hiyo imetokana na kuwatilia shaka wanafunzi walioshindwa kujitokeza kuhakikiwa.
“Tumesitisha mikopo kwa wasiohakikiwa kwa sababu hatujui kama ni wanafunzi halali au hewa. Tunataka kuwahakiki pia kwa kuwa hatujui kama wakati tunahakiki wengine walikuwa wagonjwa au wamerudia mwaka au wana sababu nyingine,”alisema.
Mei mwaka huu, Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, aliagiza kufanyika uhakiki kwenye taasisi za elimu ya juu nchini kubaini kama kuna uwepo wa wanafunzi wasiostahili kupata mikopo.
Kuanzia Mei 30, mwaka huu, HESLB ilifanya uhakiki katika vyuo 26 na tayari imeshafanya uchambuzi wa uhakiki kwa vyuo 18 kati ya hivyo.
Akizungumzia uhakiki huo, Sabi alisema ulifanywa na timu maalumu iliyoundwa na Bodi kwa kuhakikiwa mwanafunzi husika na kubaini kuwa wanafunzi 2, 739 hawakujitokeza kuhakikiwa. Aliongeza kuwa, Uchambuzi katika vyuo vinane unaendelea.
Hata hivyo, bodi hiyo haikueleza ni wanafunzi wangapi walihakikiwa katika vyuo ambavyo kazi ya uhakiki imefanyika. Alisema bodi itafanya uhakiki wa awamu ya pili ili kujiridhisha kabla ya kuwatangaza kuwa ni wanafunzi hewa na fedha ambazo zitakuwa zimeokolewa kutokana na kuwabaini wanafunzi hao.
Alisema majina ya wanafunzi ambao hawakujitokeza kuhakikiwa wakati wa uhakiki vyuoni yamewekwa kwenye tovuti ya Bodi na pia katika vyuo ambavyo vitafanya utaratibu wa awamu ya pili ya uhakiki.
Alivitaja vyuo vilivyohakikiwa, kufanyiwa uchambuzi wa awali na idadi ya wanafunzi ambao hawakujitokeza kuhakikiwa kwenye mabano kuwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (763), Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (126), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino- Mwanza( 232), Chuo Kikuu cha Mzumbe (66) na Chuo Kikuu cha Teofilo Kisaji-Mbeya (130).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-Mbeya (21), Chuo cha Mtakatifu Yohane- Dodoma (262), Chuo Kikuu cha Mkwawa (103), Chuo Kikuu cha Iringa (100) na Chuo Kikuu cha Tiba-Bugando (43), Chuo Kikuu cha Arusha (55), Chuo Kikuu cha Jordan (128), Chuo Kikuu cha Makumira- Arusha (98), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (385), Chuo cha Ufundi Arusha (22), Chuo Kikuu cha Waislamu-Morogoro (130), Chuo cha Uhasibu (57) na Chuo Kikuu cha Mount Meru (17).
Sabi alisema kutokana na kuwepo wanafunzi ambao hawajajitokeza, muda wa uhakiki umeongezwa hadiSiku 7 baadae kuanzia jana.
Wednesday, 13 July 2016
RAIS MAGUFULI AMUAHIDI MEYA WA UKAWA KUMPA KAZI
RAIS John Magufuli amemwahidi kwa utani kumpatia kazi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, endapo atafukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutokana na kusifia kazi inayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam jana, kushuhudia shughuli ya makadhibiano ya madawati ambayo yalitokana na Sh. bilioni nne ambazo zilitolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ikiwa ni mpango wake wa kubana matumizi, Rais Magufuli alisema amekuwa akivutiwa na ‘statement’ (kauli) ambazo zimekuwa zikitolewa na meya huyo.
Alisema hata alipompatia nafasi ya kuwasalimia wananchi waliofika kwenye hafla hiyo, meya huyo aliongelea masuala muhimu yenye kuleta maendeleo kwa taifa.
Rais Magufuli alisema amekuwa akifuatilia kauli za Meya Mwita na kueleza hotuba zake zimekuwa zenye dhamira ya kuleta maendeleo.
Alisema kwa mzaha, ikiwa meya huyo atafukuzwa katika chama chake yeye atamkumbuka kwa sababu bado amebakiwa na nafasi nyingi za uteuzi.
“Ninafurahi Meya Mwita, ninakupongeza sana kwa sababu nimekuwa nikisikiliza sana `statement’ zako za maendeleo, sasa sijui nikisema hivi watakubakiza au watakufukuza, ila wakikufukuza mimi nitakukumbuka kwa sababu nina nafasi nyingi bado za uteuzi,” alisema Rais Magufuli kwa utani na kusababisha watu kucheka.
Alisema viongozi wanapaswa kulenga kutatua matatizo ya wananchi na siyo kuingiza masuala ya itikadi za vyama katika kila jambo.
Awasifu Dr Tulia na Mchungaji Msigwa Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Iringa (Chadema), Peter Msigwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia, kwa kukaa pamoja katika meza kuu wakati wa hafla hiyo.
Wabunge kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walitangaza kususia vikao vya bunge vinavyoongozwa na Dk. Ackson au shughuli yoyote itakayoongozwa naye kwa madai amekuwa akiendesha vikao vya bunge kwa upendeleo na kutaka avuliwe wadhifa huo.
Rais Magufuli alisema inapofika masuala ya kuleta maendeleo ya taifa, viongozi wanapaswa kuweka kando masuala ya vyama.
Alisema hata yeye wakati akipiga kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, aliwaahidi Watanzania kuwa atawatumikia wote bila ya kuangalia vyama, kabila, dini wala rangi.
“Mmeacha vyama vyenu pembeni, mnaunga mkono maendeleo, leo unapomwona Msigwa na Tulia wapo jirani inatia moyo, ndicho tunachokitaka, nchi hii ni yetu sote, tukifanya hivyo nchi yetu itakuwa ya mfano,” alisema Rais Magufuli.
Alipoulizwa kwa kitendo chake cha kuhudhuria shughuli hiyo na kukaa meza moja na Dk, Ackson, Msigwa alisema wamefika katika hafla kama wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge.
Alisema pia walihudhuria hafla hiyo kwa sababu ni suala la maendeleo na walipaswa kushiriki ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyopangwa.
“Hii shughuli haiendeshwi wala kuandaliwa na Tulia, ni shughuli iliyoendeshwa na tume yetu na ndiyo maana tupo hapa,” alisema Msigwa.
Pia Rais Magufuli alimtaka Mbunge wa Kaliua(CUF), Magdalena Sakaya, kutoogopa kupeleka maendeleo katika jimbo lake kwa sababu maendeleo hayana chama
Mbunge huyo alisema hafla hiyo ni ya maendeleo hivyo hawakuwa na sababu ya wao kugomea.
Wabunge wa Ukawa waliwahi kukaririwa wakilalamikia kitendo cha uongozi wa Bunge kurejesha Sh. bilioni nne serikalini ili kubana matumizi.
Rais Magufuli, ambaye alikabidhiwa hundi ya fedha hizo Aprili 11, mwaka huu, alielekeza zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za
SUMAYE AKUBALI KUGOMBEA UWENYEKITI CHADEMA
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amekubali ombi la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, waliomchukulia fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kanda hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Baadhi ya viongozi hao waliojitokeza kumchukulia fomu Sumaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa chama hicho Ilala, Dk. Makongoro Mahanga na Mwenyekiti wa mkoa wa Pwani, Baraka Mwago.
Baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za Chadema Kanda Kinondoni jana, viongozi hao walielekea nyumbani kwa Sumaye maeneo ya Tondoroni Kiluvya, mkoa wa Pwani, kwa ajili ya kumkabidhi.
Baada ya kupokea fomu hizo, Sumaye alikubali ombi hilo na kuzijaza na kuahidi kurejesha leo katika ofisi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Waitara, Sumaye alisema ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi vitongojini.
Waziri Mkuu huyo mstaafu alihamia upinzania mwaka jana katika harakati za uchaguzi mkuu akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivi karibuni aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.
UINGEREZA YAPATA WAZIRI MKUU MPYA MWANAMKE BAADA YA DAVID CAMEROON KUJIUZULU
NCHI YA UINGEREZA Imepata waziri mkuu mpya Mwanamke .Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza.
Akizungumza baada ya kupokea ufungua wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza 10 Downing Street bi May amehakikishia washirika wake na mataifa ya muungano wa ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa,
Uingereza inapania kujiunga na mataifa shirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano wa mataifa huru duniani.
Amesema kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio wachache na kusahau wananchi wa kawaida.
Malkia tayari amempa idhini ya kuunda serikali mpya muda mchache tu baada ya kujiuzulu rasmi kwa aliyekuwa waziri mkuu bwana David Cameron.
May amesema kuwa serikali yake itahakikisha inawakilisha matarajio ya kila muingereza.
Aliwakumbusha wakosoaji wake maana ya jina rasmi ya chama chake ambacho ni chama cha Conservative and Unionist.
Waziri huyo mkuu ameapa kuangamiza udhalimu wa aina yeyote ima ni kwa misingi ya ubaguzi wa rangi jinsia ama kiwango cha mapato.
Bi Theresa May ni waziri mkuu wa 13 kuwahi kuiongoza Uingereza katika enzi ya Malkia Elizabeth wa pili.
Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.
Malkia tayari amempa idhini ya kuunda serikali mpya muda mchache tu baada ya kujiuzulu rasmi kwa aliyekuwa waziri mkuu bwana David Cameron.
Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret
HABARI TOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Bodi ya Mikopo imetoa orodha ya wanafunzi mbalimbali ambao hawakujitokeza ktk zoezi la uhakii la hivivi karibuni wanaofikia zaidi ya Elfu mbili, Kwa Taarifa hii bodi inawatalka wale wote ambao hawajajitokeza kuhakiki kufanya zoezi hilo ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 13 baada ya hapo atakayeshindwa atafutiwa mkopo wake rasmi na kutakiwa kurudisha aliokwishakopeshwa mara moja.
Orodha ya wanafunzi ni 2,739 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu ambao hawakuhakikiwa na ambao wanatakiwa kujitokeza ndani ya siku saba (07) kuanzia tarehe 13 Julai, 2016 ili kuhakikiwa katika sehemu watakazoelekezwa na vyuo husika. Ili kuona majina ingia http://olas.heslb.go.tz.
MAREKANI KUONGEZA ZAIDI WANAJESHI, SUDANI KUSINI
Marekani imesema itawatuma wanajeshi 40 zaidi Sudan Kusini kusaidia kulinda Wamarekani na mali ya Marekani mjini Juba.
Msemaji wa jeshi la Marekani barani Afrika, Africom, Jennifer Dyrcz amesema wanajeshi hao wa Marekani wametumwa nchini humo baada ya mapigano yaliyoanza wiki iliyopita.
Kwa sasa hali imetulia baada ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kuagiza wanajeshi wao wasitishe vita Jumatatu.
Ubalozi wa Marekani mjini Juba, kwa mujibu wa shirika la habari la AP, umesema raia wa Marekani wanaotaka kuondoka Sudan Kusini watasaidiwa kuondoka kwa ndege.
Wafanyakazi wasio muhimu sana katika ubalozi huo pia wataondolewa.
Museveni atuma jeshi kuokoa waganda Sudan Kusini
Utulivu warejea Juba, Sudan Kusini
Mashirika makubwa ya ndege yalisitisha safari za ndege kutua na kupaa kutoka Juba.
Safari za ndege za kibinafsi na za kukodisha hata hivyo zimerejelewa na ndege hizo zinatumiwa kuwaondoa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada pamoja na raia wa kigeni kutoka Juba.
Umoja wa Mataifa umesema raia 36,000 wa Sudan Kusini wametoroka makwao kutokana na mapigano na kutafuta hifadhi makanisani, katika kambi za UN na kambi za mashirika ya kutoa misaada.
MBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BURUNDI
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo#Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,” ameandika kwenye Twitter.
Bi Mossi alitetea sana haki za wanawake.
MKE AMBWAGA MKWE KATIKA KESI YA KUGOMBEA MAITI YA MUMEWE
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imeyatupilia mbali maombi ya kuzikwa Tanga mwili wa Andrew Daffa, aliyefariki dunia Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.
Mwili wa Daffa ulizuiwa kuzikwa kutokana na maombi ya kesi ya madai namba 240 ya mwaka 2016, yaliyofunguliwa na baba yake, Charles Joseph ambaye alitaka apewe kibali cha kumzika mwanaye Kijiji cha Vigiri mkoani Tanga alikozaliwa.
Mvutano huo ulijitokeza baada ya mke wa marehemu, Glory Charles kutaka kupewa haki ya kuzika mwili wa mumewe katika makaburi ya Kwa Jimmy yaliyopo Yombo Vituka.
Glory aliieleza Mahakama kuwa eneo hilo ndilo walilozika watoto wao watano, ambao alizaa na mumewe.
“Kwa sababu mume wangu alikuwa anaishi na mimi Tabata Kimanga na nilimuuguza mpaka dakika ya mwisho bila kupata msaada wa ndugu yeyote, naomba Mahakama inipe kibali cha kumzika kwani na mimi nina haki kama mke,” alidai Glory,
Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Adelf Sachore alisema Mahakama inatupilia mbali maombi ya baba wa marehemu, hivyo inaamuru mwili huo apewe mke wake.
“Maombi ya baba wa marehemu yanatupiliwa mbali, Mahakama inaamua mwili huo uzikwe walikozikwa watoto wake waliofariki dunia,” alisema.
Hakimu Sachore alisema katika kesi hiyo, Wakili wa utetezi, Daniel Buma alidai marehemu anatakiwa azikwe mkoani Tanga kwa madai kuwa ndiyo mila zao zinavyoeleza kwa sababu hana makazi ya kudumu Dar es Salaam.
Hata hivyo, Mahakama ilipokea vielelezo kutoka kwa mlalamikiwa (Glory) ambavyo ni cheti cha ndoa na picha za watoto wao waliokufa na vyeti vya watoto waliopo.
Baada ya kutolewa uamuzi huo, Glory alibubujikwa machozi ya furaha na kuomba Mahakama impe ulinzi wakati wa mazishi ya mumewe yanayotarajia kufanyika leo katika makaburi ya Yombo votuka.
MWALIMU ASHAMBULIWA KWA MAPANGA KWA KUMPA MWANAFUNZI MIMBA
Mwalimu wa Shule ya Msingi Geitasamo iliyopo Kata ya Rung’abure wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Raphael Charles (22) amenusurika kufa kwa kucharangwa mapanga kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Ikorongo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Geitasamo, Marwa Meng’anyi alisema mwalimu huyo amejeruhiwa kwa kucharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni kaka wa mwanafunzi huyo baada ya kuchukizwa na kitendo cha dada yao (jina linahifadhiwa) kukatishwa masomo kwa kupata ujauzito.
Akizungumzia tukio la kucharangwa mapanga, Mwalimu Charles alisema mkasa huo ulimkumba akiwa njiani kwenda nyumbani akiwa ameongozana na mwalimu mwenzake aliyemtaja kwa jina la Frank Batholomeo.
“Tukiwa njiani ghafla walijitokeza na kuanza kunihoji kwa nini nimempa mimba mdogo wao, kabla sijajibu mmoja wao alichomoa panga na kuanza kunishambulia akilenga kunikata shingo,” alidai Charles.
Alidai katika jitihada za kujinusuru ilimbidi kutimua mbio, lakini alianguka chini na vijana hao kufanikiwa kumfikia na kuendelea kumshambulia kwa mapanga.
Mwalimu huyo aliyefungua kesi kuhusu shambulio hilo na kupewa namba ya jalada Mug/RB/2886/2016 la kujeruhi, alidai alinusurika kuuawa baada ya mmoja wa mafundi pikipiki waliokuwa eneo jirani kujitokeza kumsaidia.
Tukio la kushambuliwa kwa mwalimu huyo limekuja huku madai dhidi yake kumpachika mimba mwanafunzi huyo yakiwa yamefikishwa mahakamani kwa shauri namba 82/2016 tangu Mei 13.
Akizungumzia kitendo chake na wanawe kumshambulia kwa mapanga mwalimu huyo, baba wa binti aliyepachikwa mimba, Chacha Masiko alidai familia imechukizwa na kesi dhidi ya mwalimu huyo kuahirishwa mara kwa mara bila wao kuelezwa sababu za msingi, huku mshtakiwa huyo akiwatambia mtaani kuwa hatafungwa.
Mwalimu aliyeshuhudia mwezake akicharangwa mapanga, Batholomeo alilaani kitendo cha wanafamilia hao kujichukulia sheria mkononi na kuomba mamlaka husika kuchukua hatua kukomesha vitendo hivyo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Kaimu Ofisa Elimu wa wilaya hiyo, Hawamu Tambwe alisema ameunda timu itakayoshirikiana na uongozi wa kijiji kuelimisha wananchi umuhimu wa kuzingatia sheria katika kushughulikia changamoto na matatizo yanayojitokeza kwenye jamii badala ya kuchukua sheria mkononi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ngh’azi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kutokana na simu yake kuita bila kupokewa, lakini mmoja wa maofisa wa polisi wilayani hapa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina alisema jeshi hilo linawasaka ndugu hao ili wafikishwe mbele ya vyombo vya
Tuesday, 12 July 2016
MFANYABIASHARA WA MILIONI 7 KWA DAKIKA APANDISHWA KIZIMBANI, ASOMEWA MASHTAKA 199.
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja.
Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.
Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha.
Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai walilazimika kubadilishana ili kuwapa muda wa kupumua.
Kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na shtaka la kutakatisha fedha, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kulingana na mashtaka yanayowakabili, hayana dhamana.
Baada ya kumaliza kuwasomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Hivyo, Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi Julai 25, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kabla ya kupandishwa kizimbani, Yusufali alitajwa na Rais Magufuli kuwa ana mashine inayotoa risiti za kielektroniki (EFD) nje ya mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzisambaza kwa wafanyabiashara wengine, hivyo kujiingizia Sh7 milioni kwa dakika.
Rais Magufuli alieleza kuwa mtandao wake unawashirikisha watumishi wa TRA na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela), hivyo kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.
Katika mashtaka hayo, Yusufali anakabiliwa na mashtaka 181 ya kughushi, mashtaka 15 ya kuwasilisha nyaraka za uongo, udanganyifu katika kulipa kodi moja, shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh15,645,944,361, huku shtaka moja tu la utakatishaji fedha ndilo likimhusisha na wenzake.
Waendesha mashtaka hao walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akighushi nyaraka za kampuni mbalimbali, kuonyesha kuwa zimesajiliwa na zinaendesha shughuli zake nchini kihalali wakati akijua siyo kweli.
Pia, walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akiwasilisha nyaraka za uongo TRA.
Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya Machi 2011 na Januari 2016, walitakatisha Sh1,895,88500 kwa kujifanya kuwa ni malipo ya mikopo waliyoipokea kwa watu mbalimbali.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa kati ya Januari 2008 na Januari 2016, mfanyabiashara huyo alifanya udanganyifu katika kuwasilisha kwa Kamishna Mkuu wa TRA taarifa ya uongo ya marejesho ya mapato, hivyo kuikosesha Serikali mapato ya kodi ya VAT zaidi ya Sh15.6 bilioni.
WAFUASI WA WASIRA WASHINDA RUFANI DHIDI YA ESTER BULAYA
Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.
Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.
Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Mohamed Gwae ilitupilia mbali kesi yao baada ya kukubaliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.
BARAZA LA TIBA ASILI LAMTUMBUA DK. MWAKA
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.
Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ,Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame.
Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai
Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ,Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.
Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya Matangazo
Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.
KAGAME AMTUMBUA WAZIRI WAKE WA AFYA.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemtimua waziri wake wa afya Dr Agnes Binagwaho aliyeongoza wizara hiyo kwa kipindi cha miaka 5.
Dr Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda lakini wadadisi wanasema kutimuliwa kwake huenda kumetokana na utendaji kazi usioridhisha na matatizo yanayoikumba wizara hiyo kwa sasa.
Tangazo lililotiwa saini na waziri mkuu Anastase Murekezi limebainisha kuwa rais wa jamhuri katika mamlaka yake amemfuta kazi waziri huyo bila kutoa maelezo zaidi.
Lakini wadadisi wanasema huenda matatizo yaliyokuwa ndani ya wizara hiyo ndicho chanzo cha waziri huyo kutimuliwa.
Wakati wa mkutano wa kitaifa mwezi Desemba mwaka uliopita,waziri huyo alikosolewa vikali na washiriki waliobainisha tatizo kubwa la ugonjwa wa malaria.
Dr Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda
Takwimu zilizopo kutoka wizara ya afya zilibainisha kuwa watu zaidi ya milioni 2.5 waliathirika na ugonjwa huo mwaka jana.
Hata hivyo katika kipindi cha miezi sita pekee ya mwaka huu wanahesabiwa wagonjwa milioni 1.,4 idadi ambayo ni kubwa sana ikilinganishwa na miaka 5 iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyokuwa katika nafasi nzuri ya kuangamiza ugonjwa huo.
Tatizo lililobainishwa na wakosoaji ni uzembe uliofanywa na wizara ya afya iliyoagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo dolla milioni 15 za Marekani.
Katika ripoti ya mkaguzi mkuu wa mali ya umma,wizara ya afya ilibainisha pengo la milioni 10 dollar za Marekani zilizotoweka.
Kadhalika swala la utendajikazi mbovu wa hospitali za serikali linalotokana na madaktari bingwa wanaozikimbia hospitali hizo.
wizara ya afya iliagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo doll
Mwezi uliopita waziri huyo alikiri kuwepo idadi kubwa ya madaktari wanaohamia katika hospitali binafsi wakikimbia mishahara midogo serikalini.
Kuna wanaoona kwamba maamzi yanayochukuliwa kuhusu hayaridhishi kukabiliana na matatizo hayo.
Kuhusu swala la malaria wizara ilikuwa na mkakati wa kutumia washauri wa afya ya uzazi katika kusaidia kutibu ugonjwa huo.
Aidha wizara ilikuwa na pendekezo kwamba waongezewe mshahara na kuruhusiwa kufanya kazi sehemu mbili.
POLISI WAMDAKA GWAJIMA
Hatimaye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye amekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa siku kadhaa alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipowasili akitokea Japan.
Baada ya Askofu Gwajima kukamatwa na Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa JNIA alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.
Akizungumzia kukamatwa kwake, Kamanda wa Polisi Uwanja wa JNIA, Martin Otieno alisema askofu huyo aliwasili saa 2.45 asubuhi akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.
Otieno alisema mara baada ya kukamatwa alipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Ni kweli tulimkamata Askofu Gwajima hapa uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kuwasili kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya na tulipomuhoji alidai kuwa alikuwa nchini Japan,” alisema Otieno.
Mwanasheria wake Peter Kibatala alisema Gwajima alifika Kituo Kikuu cha Polisi saa 4.45 asubuhi kwa mahojiano mafupi na aliruhusiwa kuondoka baada ya kujidhamini yeye mwenyewe.
“Askofu Gwajima amehojiwa leo (jana) na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu na amejidhamini yeye mwenyewe, ameruhusiwa kuondoka hivyo tunasubiri chochote kitakachoendelea,” alisema Kibatala bila kueleza mahojiano yalivyokuwa.
Askofu Gwajima alikuwa anatafutwa na polisi tangu mwezi uliopita baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake akipendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo sasa Rais John Magufuli anayashughulikia kwa mtindo wa kutumbua majipu.
Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Rais Magufuli asipewe uongozi wa chama hicho kwa sasa kama ilivyo utaratibu wa chama hicho na kwamba hilo likifanyika basi Rais abadili katiba ili mstaafu huyo aweze kufikishwa kortini.
Tangu ulipotolewa mkanda huo, makachero wa polisi wamekuwa wakipiga .kambi nyumbani kwa Askofu Gwajima kwa lengo la kumkamata lakini hawakumpata.
Baadaye ilikuja kufahamika kwamba askofu huyo alikuwa amekwenda nje ya nchi lakini haikujulikana ni nchi gani.
Hata hivyo, baada ya kutafutwa na polisi, Gwajima kupitia wakili wake Kibatala alisema atakaporejea nchini atakwenda moja kwa moja polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amekuwa akisisitiza kwamba jeshi litaendelea kumtafuta askofu huyo kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa,Interpol.
Monday, 11 July 2016
DAKTARI FEKI ANASWA WODI YA ICU HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Ulrich Matei amesema mtu huyo ameshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tuhuma zinazo mkabili na mara baad tua ya kubaini ukweli wa jambo hilo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
ETHIOPIA YAZIMA MTANDAO WA FACEBOOK NCHINI HUMO KWASABABU YA MITIHANI
Mitandao ya kijamii nchini Ethiopia imezimwa kwa sababu ya mtihani wa taifa. Waethiopia waliamka Wikiendi wakajipata hawana huduma hizo za mitandao kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber.
Serikali imefunga mitandao hiyo tangu Jumamosi usiku.
Msemaji wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa serikali ilichukua hatua hiyo kama njia ya kuzuia wanafunzi wasivurugwe na ushawishiwa mitandao hiyo ya kijamii.
Hatua hiyo vilevile imetokea majuma kadhaa baada ya baadhi ya makaratasi ya mitihani kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimu serikali kufutilia mbali mitihani hiyo iliyodukuliwa.
''Serikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano.
Tumegundua kuwa mitandao ya kijamii huvuruga kabisa ratiba ya vijana na haswa wanafunzi'', alisema msemaji wa serikali Getachew Reda .
Serikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano mitihani itakapokuwa imekamilika
Hatu hiyo bila shaka imewaudhi wanaharakati wa kupigania uhuru wa habari nchini Ethiopia.
Mwanabloggu mashuhuri Daniel Berhane amechapisha kwenye mtandao wake wa Twit
KOREA YA KASKAZINI YAKATA MAWASILIANO NA MAREKANI
Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini, wanasema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.
Korea Kaskazini inasema kuwa utawala wa Washington tayari umefahamishwa sababu ya hatua hiyo.
Aidha Korea imesema kuwa maswala ambayo bado yanajadiliwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wamarekani wawili sasa yatajadiliwa chini ya sheria kali za kivita.
Korea kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza vita dhidi yao .
Korea Kaskazini inasema hatua hiyo imeafikiwa katika kile kinachotajwa kama sheria ya kivita.
Shirika hilo la sereikali aidha linasema kuwa imeafikia hatua hiyo baada ya Marekani kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imeapa kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga roketi zake za masafa marefu.
Marekani na Korea Kusini zimetangaza mipango ya kuweka Mfumo wa ulinzi wa Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unaolenga kudungua makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini.
Korea Kaskazini imeudhika na Marekani kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Korea kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza vita dhidi yao .
Hata hivyo haijajulikana Marekani na Korea Kaskazini zitaiweka wapi mtambo huo wa ulinzi wa kisasa na yupi kati ya washirika hao wawili watauendesha mtambo huo katikaaunganisha wapenzi wa Kiislamu wadukuliwa
MTOTO WA MIAKA MINNE AUAWA NA KUTUPWA KISIMANI
Mtoto wa kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa.
Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita.
Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani alisema binti yake alitoweka nyumbani saa tano asubuhi, wakati wakiwa pamoja wakitazama televisheni.
“Alitoka nje kama anaenda kucheza na wote hatukuwa na wasiwasi. Baada ya saa moja tulishtuka baada ya kutomuona, hivyo ikabidi tuanze kumtafuta,” alisema.
Alisema walitoa taarifa polisi na kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio hadi jana mwili wake ulipokutwa umening’inizwa kwenye kisima cha nyumba ya jirani yao.
“Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni kavu na ana majeraha,” alisema.
Alisema kisima hicho kina tundu dogo ambalo huenda wauaji walijitahidi kuusukumiza mwili huo ili ionekane kama amefia humo ikashindikana.
Alisema mpaka juzi mchana, kilikuwa kikitumika na kuwa huenda mwili huo ulining’inizwa usiku wa kuamkia jana.
Baadhi ya majirani waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Kamanda wa Polisi Temeke, Andrew Satta alisema wanaendelea na uchunguzi: “Taarifa zilizopo ni kwamba amekufa maji lakini kwa hayo mazingira mengine tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi".
Sunday, 10 July 2016
NAIBU SPIKA AFUNGUKA RASMI KUHUSU HOJA YA UKAWA
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amesema hoja ya wabunge wa Ukawa kutaka aenguliwe kwenye wadhifa huo inafanyiwa kazi na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo iwapo itaridhia, itarejeshwa bungeni kupigiwa kura ambazo hata hivyo, hazitatosha kwa uchache wao.
Dk Tulia alisema hayo jana wakati akihojiwa na Tido Mhando katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Azam TV.
“Hoja ikishakuja bungeni hapo sasa huwa ni kampeni na baadaye kupigiwa kura. Kwa kuwa waliopeleka hoja ni wabunge wa upinzani, hivyo wanatakiwa kufikisha idadi fulani ambayo kiuhalisia wao kwa sasa hawana,” alisema.
Kwa karibu mwezi mzima kwenye Bunge la Bajeti, wabunge wa Ukawa walimsusia Dk Tulia na walikuwa wakitoka bungeni kila alipoingia, tayari wameanzisha mchakato wa kumuondoa madarakani kwa madai kuwa hawatendei haki na anaminya demokrasia ndani ya Bunge.
Dk Tulia alisema Katiba inatambua kwamba kiongozi aliyechaguliwa anaweza kuondolewa madarakani na wale waliomchagua, hivyo wabunge wa upinzani wametumia haki yao ya msingi na kinachosubiriwa ni hoja yao kufanyiwa kazi.
“Kanuni imeweka wazi na msingi ule umejengwa kwenye Katiba kwa sababu inatambua wale waliomchagua kiongozi wasiporidhika naye wanaweza kumuondoa madarakani. Nafarijika kuona wanachukua hatua, hivyo mimi sina malumbano nao,” alisema.
Hakuna maridhiano Dk Tulia alisema hakuna maridhiano yanayotakiwa baina yake na wabunge wa Ukawa kwa kuwa hana malumbano nao, bali kanuni na taratibu zinafuatwa kufanikisha hoja yao ya kumuondoa madarakani.
Naibu Spika huyo alisema maridhiano huwapo baina ya watu wanaolumbana na kwamba, baina yao hakutakuwa na suala hilo.
MBOWE APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA BAVICHA KUZUIA MKUTANO WA CCM DODOMA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kusitisha mpango wa vijana wa chama hicho kwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea. Badala yake, Mbowe amesema wataendelea kusaka haki ya kufanya mikutano ndani na nje ya nchi.
Sambamba na uamuzi huo, chama hicho kimetaka viongozi sita wa Baraza la Vijana (Bavicha) wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuachiwa mara moja.
Mbowe alitoa tamko hilo jana wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha, katika mkutano wa mameya na wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa).
Sababu za kusitisha Mbowe alisema wamewataka vijana wa Chadema nchi nzima ambao walianza kujiandaa kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano huo wa Julai 23 kutokwenda kwa sababu polisi wamepewa maagizo ya kuwapiga na kuwajeruhi, hivyo wao hawataki kupambana nao.
“Nawataka vijana wote wa Chadema waliokuwa wanajiandaa kwenda Dodoma wasitishe na wasubiri maelekezo mapya ya Chadema,” alisema Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema wana taarifa Jeshi la Polisi limejipanga kuwanyima dhamana viongozi wa Bavicha hadi baada ya mkutano wa CCM, ingawa viongozi wote wa chama hicho hawana hofu ya kukaa mahabusu.
Aliwataka vijana hao kutokwenda Dodoma na wawaache CCM waendelee na mkutano wao kwa kuwa Chadema haina hofu na mkutano wa chama hicho, bali walitaka dunia ione jinsi polisi wanavyofanya kazi kwa maelezo ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi.
“Wakati sisi tunazuiwa kufanya siasa, Rais anafanya siasa, Waziri Mkuu anafanya siasa, mawaziri wanafanya siasa, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya siasa jambo ambalo si sahihi,” alisema.
Alisema lengo la Bavicha kwenda Dodoma ni kuchoshwa na uonevu wa kuzuiwa kufanya mikutano ya ndani na hadhara wakati CCM wanaendelea na mikutano yao.
“Waliona pengine itakuwa busara washinikize polisi kuona maagizo yao ya kuzuiwa mikutano yanatekelezwa kwa wote,” alisema.
Alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa kufuata taratibu kwa kutoa haki sawa kwa wote, kwa kuruhusu vyama vyote kufanya mikutano yao.
Apinga tamko la Mwigulu Kuhusu tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mikutano hiyo, Mbowe alisema hawakulielewa tamko hilo la Rais, kuwa mikutano ambayo imezuiwa ni ya hadhara na maandamano na si ya ndani.
Alisema mikutano ya ndani ya chama hicho imezuiwa kwani Chadema Wilaya ya Kahama walikuwa na mkutano wa ndani wa uchaguzi ambao umezuiwa.
Alisema mkutano wa ndani na wabunge wa Chadema mkoani Shinyanga ulizuiwa na pia mahafali za Vijana wa Vyuo Vikuu wa Chadema (Chaso).
“Lakini wakati haya yanafanyika, CCM waliendelea na mikutano yao na mahafali yao,” alisema.
Alisema Chadema itaendelea kudai haki ya mikutano na maandamano katika mahakama za ndani na nje ikiwamo ya Afrika ya Mashariki.
Viongozi wa madiwani Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alichaguliwa kuwa katibu wa madiwani wote wa chama hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Moses Matiku alichaguliwa kuwa mnadhimu wao. Wote hao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu Chadema.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Saturday, 9 July 2016
BAVICHA WAITANGULIA CCM DODOMA, WAISHIA RUMANDE
JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia viongozi watatu wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Taifa, kwa uchochezi na kuikashifu serikali.
Pia viongozi hao wanadaiwa kuvaa fulana zenye maandishi demokrasia imenyongwa, huku nyingine zikiandikwa dikteta uchwara.
Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Patrobas Katambi, Katibu wa Bavicha-Taifa, Julius Mwita na Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya, George Tito.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema watuhumiwa hao watashikiliwa mpaka Jumatatu watakapofikishwa mahakamani.
“Hawatadhaminiwa mpaka Jumatatu, watakapofikishwa mahakamani,” alisema.
Kamanda Mambosasa alisema kitendo cha viongozi hao kuvaa fulana inayosema demokrasia imenyongwa, inamaanisha serikali inanyonga demokrasia, jambo ambalo ni la uchochezi.
MTATIRO AMFUNGIA MILANGO PROF. LIPUMBA
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro amesema hana mpango wa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho, licha ya kuwepo kwa msukumo mkubwa wa kumtaka agombee.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, Mtatiro alisema kwa kipindi kirefu amekuwa akipata msukumo kutoka kwa viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya, wabunge, wafuasi na makada wa chama hicho kumtaka ashiriki katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti.
“Katika kipindi chote cha misukumo hiyo nimekuwa nikiwajibu wahusika wote kuwa “sina nia ya kuchukua uongozi wa juu wa chama” kwa sababu bado nahitaji muda wa kujiimarisha,” alisema Mtatiro katika taarifa yake.
Alisema hata aliposhauri kuwa Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba anapaswa kupumzika wapo walioona kuwa anatumia nafasi hiyo kuutaka uenyekiti wa CUF jambo ambalo alisema si kweli.
Aidha, Mtatiro alisisitiza kuwa hajawahi kuwa na nia ya kuutaka uenyekiti wa CUF lakini hadi sasa msimamo wake ni kuwa haungi mkono Profesa Lipumba kurudi katika nafasi yake kwa sababu siasa za sasa zinahitaji viongozi wapya na wanaoweza kutazama mambo kisasa kwa mahitaji ya kizazi kipya.
“... Na kwa sababu Profesa Lipumba anayo heshima kubwa kwa CUF na watanzania, ni muhimu zaidi alinde heshima yake na abaki kuwa mshauri mkuu wa chama. CUF ya sasa inahitaji mwenyekiti imara anayeweza kukisimamia chama na kikajijenga lakini pia mwenye uwezo na ushawishi wa kufanya siasa za ushirikiano na haki,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mtatiro alisema anawatakia kila la heri wanachama wa CUF ili waweze kuchagua mwenyekiti mzuri kwa ajili ya kukiendeleza chama hicho, na kusisitiza kuwa jukumu lake litaendelea kukisaidia chama katika masuala mbalimbali ya kiushauri.
MBINU ZA BAVICHA KUZUIA MKUTANO WA CCM DODOMA TAR 23/07/2016 ZAGONGA MWAMBA
ONYO limetolewa kwa vyama vya siasa vinavyojaribu kusuguana na Jeshi la Polisi kukumbuka kuwa hilo ni jeshi, ambalo liko tayari kutumia nguvu na rasilimali zote, kuhakikisha raia na mali zao ni salama.
Jeshi hilo pia limesema halihitaji msaada wowote kutoka kwa vyama vya siasa na wakihitaji msaada, wataomba kutoka katika vyombo vingine vya kiusalama.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya, baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kudai kuandaa vijana kwenda Dodoma kusaidia polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu.
“Nawaasa vijana, watoto msisuguane na jeshi, si busara kusuguana na jeshi, fanyeni mambo ambayo nchi itakuwa salama, polisi itatumia nguvu zote pamoja na rasilimali tulizonazo kuhakikisha raia na mali zao wanabaki salama.
“Hakuna suala la kusaidia Jeshi la Polisi au nini, sisi tunajitosheleza wenyewe, kama tutahitaji msaada wowote katika ulinzi basi msaada huo tutauomba kwa vyombo vingine vya ulinzi, ambavyo vina mafunzo kama sisi na si kwa vyama vya siasa,” alionya.
Alisema anatumia neno ‘ole’ kwa watu watakaojaribu kuvuruga amani kwa madai ya kusaidia kuzuia mkutano, kwamba polisi haitasita kuchukua hatua.
Alifafanua kuwa Jeshi la Polisi halijazuia mikutano yote ya ki.siasa na kwamba limelazimika kutoa ufafanuzi, kutokana na kuibuka kwa tafsiri tofauti kutoka kwa vyama vya siasa na makundi ya watu, baada ya polisi kutoa tamko Juni 7 mwaka huu la kupigwa marufuku mikutano ya hadhara.
Mssanzya alisema hakuna sehemu yoyote tamko hilo lilipiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa iliyofanywa kwa mujibu wa kanuni za vyama husika.
“Ndio maana baada ya tamko lile, baadhi ya vyama vimefanya na kupanga kufanya mikutano ya kiutendaji na kiutawala bila kuingiliwa au kuzuiwa na Jeshi la Polisi,” alisema Mssanzya akitolea mfano mkutano wa Bavicha kuzungumza na vyombo vya habari Julai 3, mwaka huu.
Alisema shughuli ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Chadema (Chaso) iliyopanga kufanyika Dodoma na ule wa chama cha ACT Wazalendo, ilizuiliwa kwa sababu ujumbe uliolengwa katika shughuli hizo, ulikuwa wa uchochezi na haikuwa mikutano ya kiutendaji au kiutawala.
Hata hivyo alisema pamoja na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano hiyo ya ndani, bado jeshi hilo lina mamlaka ya kuzuia pale itakapobainika ina lengo la kuhamasisha uchochezi au kuharibu amani na utulivu.
Alitoa mwito kwa wananchi wote na vyama vya siasa, kuheshimu sheria za nchi na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zake unaenda kuimarika
MHASIBU MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA ASIMAMISHWA KAZI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma zinazomkabili.
Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha malipo hayo hewa.
NDOA ZA UTOTONI TANZANIA ZAKOMA RASMI
Mahakama kuu nchini Tanzania jan imeidhinisha umri halisi wa kuolewa kwa mtoto wa kike kuwa miaka 18. Wasichana wenye umri wa miaka 14 huolewa kwa ridhaa ya wazazi wao.
Mahakama kuu imetoa muda wa mwaka mmoja kuhakikisha kuwa Serikali inasahihisha sheria ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kinachoruhusu Mtoto wa kike kuozwa akiwa na umri miaka 14
Wasichana wanaoolewa katika umri huu mara nyingi wanakabiliwa na unyanyasaji wa majumbani sambamba na kutengwa na jamii huku wakipewa nafasi ndogo kwa ajili ya elimu na ajira.
Huu ni ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa Tanzania katika kupigania haki za watoto na sasa itakuwa rahisi kuwaokoa wasichana wanaoathirika na utamaduni wa kuozeshwa wakiwa wadogo.
Uamuzi huu umekuja wakati Bunge kupitisha sheria ya kifungo cha miaka 30 ama faini ya dola 2500 kwa mwanaume atayebainika kumuoa ama kumpa mimba mwanafunzi.Hata hivyo sheria hii inawatenga maelfu ya wasichana ambao si wanafunzi.
KOREA YA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA LINGINE HATARI.
Maafisa wa kijeshi nchini Korea Kusini wanasema Korea Kaskazini imejaribu kurusha kombora kutoka kwa manowari ya kivita na kukiuka vikwazo vya kimataifa
Wanasema kuwa kombora hilo hatahivyo lilifeli muda mfupi baada ya kurushwa
Urushaji huo wa kombora unajiri baada ya Korea Kusini na Marekani kukubaliana kuweka mitambo ya kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un na maafisa wake wa kijeshi
Mitambo hiyo ina uwezo wa kutambua makombora na kisha kuyadungua.
Nchi hizo mbili ziliafikia mpango huo baada ya majaribio kadha ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini mapema mwaka huu.
ASKARI 5 WA JESHI LA MAREKANI WAUAWA KATIKA MAANDAMANO MAKUBWA YA KUPINGA MAUAJI YA WATU WEUSI HUKO DALLAS
ASKARI watano wa Jeshi la Polisi jana waliuawa kwa kudunguliwa na mtu asiyejulikana mitaa ya Dallas nchini Marekani, wakati wa maandamano makubwa ya kupinga mauaji ya watu wawili weusi yaliyofanywa na askari wa kizungu wiki hii.
Ripoti ya jeshi la polisi limeeleza kuwa mbali na askari hao waliouawa, askari wengine wanne wa jeshi la polisi na afisa mmoja wa usafiri wa mwendo kasi walijeruhiwa vibaya.
Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Dallas, David Brown aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Polisi walikuwa katika hatua za kumtia nguvuni mtuhumiwa mmoja kutokana na tukio hilo, na kwamba wakati wanajaribu kuzungumza naye akiwa mbali akiwa ameshikilia bunduki alieleza kuwa alikuwa amekasirishwa na vitendo vya mauaji ya polisi wazungu dhidi ya weusi yaliyofanyika Alhamisi.
“Alisema alitaka kuwaua wazungu,” Brown alieleza.
Baada ya majibizano ya risasi na mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Micah Xavier Johnson, polisi walituma robot lenye vilipuzi vilimuua.
Thursday, 7 July 2016
BREAKING NEWS: RAIS AFANYA UTEUZI WA WAKURUGENZI WAPYA 120.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 07 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
ARUSHA Arusha Jiji – Athumani Juma Kihamia Arusha DC – Dkt. Wilson Mahera Charles Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko Longido DC – Jumaa Mohamed Mhiwapijei Meru DC – Kazeri Christopher Japhet Monduli DC – Stephen Anderson Ulaya Ngorongoro DC – Raphael John Siumbu
DAR ES SALAAM Dar es salaam Jiji – Siporah Jonathan Liana Kinondoni Manispaa – Aron Titus Kagurumjuli Temeke Manispaa – Nassibu Bakari Mmbaga Ilala Manispaa – Msongela Nitu Palela Kigamboni Manispaa – Stephen Edward Katemba Ubungo Manispaa – Kayombo Lipesi John
DODOMA Dodoma Manispaa – Dkt. Leonard M. Masale Kondoa DC – Kibasa Falesy Mohamed Kondoa Mji – Khalifa Kondo Mponda Mpwapwa DC – Mohamed Ahamed Maje Kongwa DC – Mhandisi Ngusa Laurent Izengo Chemba DC – Semistatus Hussein Mashimba Chamwino DC – Athuman Hamis Masasi Bahi DC – Rachel Marcel Chuwa
GEITA Bukombe DC – Dionis Maternus Nyinga Chato DC – Mhandisi Joel Bahahari Geita DC – Ally Abdallah Kidwaka Geita Mji – Modest J. Apolinaly Mbogwe DC – Mahwago Elias Kayandabila Nyang’wale DC – Carlos K. Gwamagobe
IRINGA Iringa Manispaa – William Donald Mafwele Mafinga Mji – Saada S. Mwaruka Mufindi DC – Riziki Salas Shemdoe Iringa DC – Robert Mgendi Magunya Kilolo DC – Aloyce Kwezi
KAGERA Biharamulo DC – Wende Israel Ng’ahala Bukoba DC – Abdulaaziz Jaad Hussein Bukoba Manispaa – Makonda Kelvin Stephen Karagwe DC – Godwin Moses Kitonka Kyerwa DC – Shedrack M. Mhagama Missenyi DC – Limbe Berbad Maurice Muleba DC – Emmanuel Shelembi Luponya Ngara DC – Aidan John Bahama
KATAVI Mlele DC – Alex Revocatus Kagunze Mpimbwe DC – Erasto Nehemia Kiwale Mpanda DC – Ngalinda Hawamu Ahmada Mpanda Manispaa – Michael Francis Nzyungu Nsimbo DC – Joachim Jimmy Nchunda
KIGOMA Buhigwe DC – Anosta Lazaro Nyamoga Kakonko DC – Lusubilo Joel Mwakabibi Kasulu DC – Godfrey Msongwe Masekenya Kasulu Mji – Fatina Hussein Laay Kigoma Ujiji – Manispaa –Judethadeus Joseph Mboya Kigoma DC – Hanji Yusuf Godigodi Kibondo DC – Shelembi Felician Manolo Uvinza DC – Weja Lutobola Ng’olo
KILIMANJARO Manispaa ya Moshi – Michael Nelson Mwandezi Hai DC – Yohana Elia Sintoo Siha DC – Valerian Mwargwe Juwal Same DC – Shija Anaclaire Mwanga DC – Golden A. Mgonzo Rombo DC – Magreth Longino John Moshi DC – Emalieza Sekwao Chilemeji
LINDI Kilwa DC – Bugingo I. N. Zabron Lindi DC – Samwel Warioba Gunzar Lindi Manispaa – Jomaary Mrisho Satura Liwale DC – Justine Joseph Monko Nachingwea DC – Bakari Mohamed Bakari Ruangwa DC – Andrea Godfrey Chezue
MANYARA Babati Mji – Fortunatus Hilario Fwema Hanang DC – Bryceson Paul Kibasa Mbulu DC – Festi Fungameza Fwema Mbulu Mji – Anna Philip Mbogo Simanjiro DC – Yefred Edson Myezi Kiteto DC – Tamim Kambona Babati DC – Hamis Iddi Malinga
MARA Manispaa ya Musoma – Fidelica Gabriel Myovela Bunda DC – Amos Jeremiah Kusaja Bunda Mji – Janeth Peter Mayanja Butiama DC – Solomon Kamlule Ngiliule Musoma DC – Flora Rajab Yongolo Serengeti DC – Juma Hamsini Seph Rorya DC – Charles Kitanuru Chacha Tarime DC – Apoo Castro Tindwa Tarime Mji – Hidaya Adam Usanga
MBEYA Busokelo DC – Eston Paul Ngilangwa Chunya DC – Sofia Kumbuli Kyela DC – Mussa Joseph Mgata Mbarali DC – Kivuma Hamis Msangi Mbeya DC – Ameichiory Biyengo Josephat Mbeya Jiji – Zacharia Nachoa Ntandu Rungwe DC – Loema Isaya Peter
SONGWE Momba DC – Adrian Jovin Jungu Tunduma Mji – Valery Alberth Kwemba Mbozi DC – Edna Amulike Mwaigomole Ileje DC – Haji Mussa Mnasi Songwe DC – Elias Philemon Nawela
MOROGORO Gairo DC – Agnes Martin Mkandya Kilombero DC – Dennis Lazaro Londo Ifakara Mji – Francis Kumba Ndulane Kilosa DC – Kessy Juma Mkambala Morogoro DC – Sudi Mussa Mpili Morogoro Manispaa – John Kulwa Magalula Mvomero DC – Florent Laurent Kyombo Ulanga DC – Audax Christian Rukonge Malinyi DC – Marcelin Rafael Ndimbwa
MTWARA Mtwara DC – Omari Juma Kipanga Mtwara Mikindani Manispaa –Beatrice Dominic Kwai Masasi Mji – Gimbana Emmanuel Ntayo Masasi DC – Mkwazu M. Changwa Nanyumbu DC – Hamis Hassan Dambaya Newala DC – Mussa Mohamed Chimae Newala Mji – Andrew Frank Mgaya Tandahimba DC – Said Ally Msomoka Nanyamba Mji – Oscar Anatory Ng’itu
MWANZA Mwanza Jiji – Kiomoni Kibamba Kiburwa Ilemela Manispaa – John Paul Wanga Kwimba DC – Pendo Anangisye Malabeja Magu DC – Lutengano George Mwalwiba Misungwi DC – Eliud Leonard Mwaiteleke Ukerewe DC – Tumaini Sekwa Shija Buchosa DC – Crispian Methew Luanda Sengerema DC – Magesa M. Boniphace
NJOMBE Njombe Mji – Iluminata Leonald Mwenda Makambako Mji – Paul Sostenes Malala Makete DC – Francis Emmanuel Namaumbo Njombe DC – Monica Peter Kwiluhya Ludewa DC – Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija Wanging’ombe DC – Amina Mohamed Kiwanuka
PWANI Bagamoyo DC – Azimina A. Mbilinyi Chalinze DC – Edes Philip Lukoa Kibaha DC – Tatu Seleman Kikwete Kibaha Mji – Jenifer Christian Omolo Kisarawe DC – Mussa L. Gama Mafia DC – Erick Mapunda Mkuranga DC – Mshamu Ally Munde Kibiti DC – Alvera Kigongo Ndabagoye Rufiji DC – Salum Rashid Salum
RUKWA Kalambo DC – Simon Ngagani Lyamubo Sumbawanga DC – Nyangi John Msemakweli Sumbawanga Manispaa – Hamid Ahmed Njovu Nkasi DC – Julius M. Kaondo
RUVUMA Mbinga DC – Gumbo Samanditu Gumbo Mbinga Mji – Robert Kadaso Mageni Namtumbo DC – Christopher Michael Kilungu Nyasa DC – Oscar Albano Mbuzi Songea DC – Simon Michael Bulenganija Madaba DC – Shafi Kassim Mpenda Tunduru DC – Abdallah Hussein Mussa Songea Manispaa – Tina Emelye Sekambo
SHINYANGA Kishapu DC – Stephen Murimi Magoiga Msalala DC – Berege Sales Simon Shinyanga DC – Mark Emmanuel Malembeka Kahama Mji – Anderson David Msumba Shinyanga Manispaa – Lewis Kweyemba Kalinjuna Ushetu DC – Michael Augustino Matomola
SIMIYU Bariadi DC – Abdallah Mohamed Malela Bariadi Mji – Melkizedek Oscar Humbe Itilima DC – Mariano Manyingu Maswa DC – Fredrick Damas Sagamiko Busega DC – Anderson Njiginya Meatu DC – Said F. Manoza
SINGIDA Ikungi DC – Rustika William Turuka Iramba DC – Linno Pius Mwageni Mkalama DC – Martin Msuha Mtanda Manyoni DC – Charles Edward Fussi Itigi DC – Luhende Pius Gerald Singida DC – Rashid Mohamed Mandoa Singida Manispaa – Kizito L. Brava
TABORA Igunga DC – Revocatus Lubigili Kuuli Kaliua DC – John Marco Pima Nzega DC – Jacob James Mtalitinya Nzega Mji – Phillimon Mwita Magesa Sikonge DC – Simon Saulo Ngatunga Tabora Manispaa – Bosco Addo Ndunguru Urambo DC – Magreth Nakainga Tabora -Uyui – Hadija Maulid Makuani
TANGA Tanga Jiji – Daudi R. Mayeji Korogwe DC – George John Nyaronga Korogwe Mji – Jumanne Kiangoshauri Muheza DC – Luiza Osmin Mlelwa Handeni Mji – Keneth K. Haule Handeni DC – William Methew Mafukwe Pangani DC – Sabas Damian Chambasi Mkinga DC – Mkumbo Emmanuel Barnabas Bumbuli DC – Peter Isaiah Nyalali Kilindi DC – Clemence Andagile Mwakasenda Lushoto DC – Kazimbaya Makwega Adeladius
Wakurugenzi wote walioteuliwa wametakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es salaam siku ya Jumanne July 12 2016 saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
Subscribe to:
Comments (Atom)